IQNA

Kikao cha Qur'ani cha burudani salama chafanyika mjini Riyadh

13:59 - April 23, 2009
Habari ID: 1768741
Kikao cha Qur'ani cha Burudani ya Amani na Salama maalumu kwa wasichana na wanawake walio na umri wa kati ya miaka 13 hadi 30 kilifunguliwa jana Jumatano mjini Riyadh Saudi Arabia na Idara ya Masuala ya Wanawake ya Kituo cha Masomo ya Qur'ani Tukufu.
Akizungumzia suala hilo, Sheikhatu as-Salman mkuu wa kituo hicho amesema kuwa, ratiba ya kikao hicho cha siku mbili itajumuisha masuala mbalibali zikiwemo hotuba zinazohusu masuala ya Qur'ani, mashindano ya burudani, futuhi na tamthiliya, filamu za kweli, maonyesho ya vitabu vya kidini na kasida. Amesema kikao hicho kimeandaliwa kwa ajili ya kuwafahamisha wasichana na wanawake burudani salama za Kiislamu, kugundua vipawa vya washiriki, kutumia vizuri nafasi za wasichana na wanawake katika familia na kuimarisha moyo wao wa kuhisi kuwa na majukumu katika jamii. 392944
captcha