Jumuiya hiyo imesema kuwa imebuni mbinu hiyo mpya ya mafunzo ya Qur'ani kupitia mtandao wa intaneti kwa shabaha ya kustawisha zaidi mafunzo ya elimu ya Qur'ani na kupanua harakati za mafunzo hayo.
Mwenyekiti wa jumuiya ya Kheri na Kuhifadhisha Qur'ani ya Saudia Aidha al Aufi amesema kuwa hii leo mtandao wa intaneti umekuwa wenzo sahali unaotayarisha uwanja mzuri wa kueneza na kupanua mafunzo ya Qur'ani na kuongeza kuwa jumuiya hiyo kwa sasa ina walimu 2900 wa Qur'ani wa kiume na 2800 wa kike.
Al Aufi ametilia mkazo udharura wa kusaidiwa jumuiya zinazojihusisha na masuala ya Qur'ani na akasema kuwa kustawishwa kwa vituo hivyo ni moja ya njia za kuwaamsha vijana katika nchi za Kiisalmu. Amesema kuwa kutumia teknolojia ya kisasa na walimu wenye uzoefu na tajriba ni miongoni mwa njia nzuri za kuwaunganisha vijana na kitabu kitukufu cha Qur'ani. 392175