Shirika la Elimu, Sayansi na Utamaduni la Jumuiya ya Nchi za Kiislamu ISESCO limepanga kuitisha kongamano la Haki za Watoto katika Uislamu hapo tarehe 27 hadi 29 mwezi huu wa Aprili katika mji mkuu wa Jordan Amman.
Mkutano huo utachunguza muundo na sababu za kupevuka mapema watoto wadogo na mchango wa chekechea na vituo vya kulea watoto wadogo.
Lengo la kongamano hilo limetajwa kuwa ni kuwaelimisha viongozi wa vituo vya kulea watoto mbinu mpya za malezi, mambo yanayopaswa kutambuliwa na waalimu wa vituo hivyo kwa ajili ya kutoa malezi sahihi ya Kiislamu na jinsi ya kutumia vigezo vya kielimu.
Katika upande mwingine shirika la ISESCO litashiriki katika kikao cha tatu cha kimataifa cha Utafiti wa Malezi na Mfungamano wa Kijamii mahsusi kwa nchi za kandokando ya bahari ya Mediterania.
Kikao hicho kitafanyika nchini Italia na kuhudhuriwa na wawakilishi wa nchi za Ufaransa, Algeria, Uhispania, Tunisia na mwenyeji Italia. 393167