Kwa mujibu wa mwandishi wa IQNA nchini Uturuki, kongamano hilo limehudhuriwa na wanasiasa na wasomi muhimu wa Palestina kama vile Raeed Salah, Mkuu wa Harakati ya Kiislamu ya Palestina pamoja na waandishi na wasomi kutoka maeneo mbali mbali duniani.
Kongamano hilo limejadili masuala kama vile hatari zinazoukabili msikiti wa Al Aqsa, utambulisho wa Kiarabu, Kiislamu na kihistoria wa msikiti huo na nafasi yake katika Uislamu.
Aidha washiriki walijadili jitihada za kuyanusuru matukufu ya Kiislamu na Kikristo katika Quds Tukufu ambayo yanakabiliwa na hujuma ya wavamizi Wazayuni.
Kongamano la Kimataifa la Kuutetea Mji wa Baitul Muqaddas na Msikiti wa Al Aqsa linafanyika mjini Istanbul katika hali ambayo utawala haramu wa Israel unaendelea kuchimba chini ya msikiti wa Al Aqsa kwa lengo la kuuharibu msikiti huo. Suala hilo limeibua hisia kali miongoni mwa Waislamu wote duniani ambao wametaka hatua madhubuti zichukuliwe kuzuia njama za utawala ghasibu wa Israel za kuuharibu msikiti wa Al Aqsa na kuuyahudisha mji wa Baitul Muqaddas. 393939