IQNA

Chuo kikuu cha Kikristo cha Thailand chakataa mwalimu Muislamu

9:33 - April 26, 2009
Habari ID: 1769729
Chuo Kikuu cha Kikristo cha Thailand kimepinga suala la mwalimu Muislamu kufundisha chuoni hapo, hatua ambayo imetajwa kuwa ni ya kibaguzi.
Mwalimu Muislamu Bi Rashinda aliwalisha mashtaka yake katika Wizara ya Elimu ya Thailand baada ya kukataliwa kufunza katika Chuo Kikuu cha Kikristo cha nchi hiyo kwa sababu za kidini.
Bi Rashida ametaka kuheshimia haki sawa ya kufundisha kati ya Waislamu na wasiokuwa Waislamu nchini Thailand.
Chuo Kikuu cha Kikristo cha Thailand kimetetea hatua hiyo ya kibaguzi kwa kudai kuwa ni kituo cha Kikristo na kwamba kuwepo mwalimu Muislamu chuoni hapo kutaathiri shughuli za kidini na mbinu za kufunza za walimu wengine. 391369

captcha