Kikao cha kimataifa cha 'Usanifu Majengo wa Nchi za Kiislamu na Nafasi yake katika Ustawi wa Kiutamaduni, Kijamii na Kiuchumi' kimepangwa kufanyika mwaka ujao wa 1431 Hijiria mjini Riyadh Saudi Arabia.
Kikao hicho kimeandaliwa na Kamisheni ya Utalii na Athari za Kihistoria ya nchi hiyo. Kwa mujibu wa shirika la habari la SPA Salman bin Abdul Aziz mkuu wa kamisheni hiyo na pia mmoja wa waandaaji wa kikao hicho amesema kuwa kikao hicho kitaandaliwa katika fremu ya mpango wa serikali ya Saudi Arabia wa kulinda urithi wenye thamani kubwa wa historia ya Kiislamu. Amesema maonyesho ya usanifu majengo wa Kiislamu yataandaliwa pambizoni mwa kikao hicho cha kimataifa ambapo nchi tofauti za Kiislamu na taasisi pamoja na mashirika ya kiutamaduni ya kimataifa yatashiriki.
Hatua hiyo ya Saudi Arabia imechukuliwa katika hali ambayo tokea kuasisiwa kwa serikali ya Kiwahabi nchini humo, makundi ya Kiwahabi yameharibu athari nyingi na zenye thamani kubwa za historia ya Kiislamu. 393971