Kituo cha Utamaduni wa Kiislamu cha mjini Brussels, siku ya Jumamosi kiliandaa mashindano ya kuhifadhi na kusoma Qur'ani Tukufu kwa mfumo wa tajweed, ambayo yamepewa jina la Amir wa Kuwait.
Gazeti la al-Qabas linalochapishwa nchini humo limesema kuwa lengo la kuandaliwa mashindano hayo ni kuwafanya Waislamu waliowachache waishio nchini Ubelgiji kusoma na kuhifadhi Qur'ani Tukufu.
Mashindano hayo ya kuhifadhi na kusoma Qur'ani Tukufu kwa mbinu ya tajweedi na ambayo yanasimamiwa na ubalozi wa Kuwait nchini Ubelgiji, yanafanyika katika hatua zifuatazo: kuhifadhi Qur'ani nzima kwa mbinu ya tajweedi, juzuu 20, juzuu 15, juzuu 4 na hatimaye juzuu 5. 393852