IQNA

Kikao cha 'Uchumi wa Kiislamu' kufanyika nchini Malaysia

10:19 - April 27, 2009
Habari ID: 1770125
Ekmeleddin Ihsanoglu, Katibu Mkuu wa Jumuiya ya Nchi za Kiislamu OIC amesema kuwa atashiriki katika kikao cha kimataifa cha 'Uchumi wa Kiislamu na Taaluma ya Uchumi' cha nchi wanachama wa jumuiya hiyo ambacho kimepangwa kufanyika hivi karibuni mjini Kuala Lumpur Malaysia.
Kwa mujibu wa OIC, Ihsanoglu atazungumza katika kikao cha ufunguzi wa kikao hicho ambacho kimeandaliwa kwa ushirikiano wa Chuo Kikuu cha Kiislamu cha Malaysia, kuhusiana na nafasi ya umoja huo katika kuimarisha ushirikiano wa kiuchumi kati ya nchi za Kiislamu.
Ihsanoglu pia atafungua pambizoni mwa kikao hicho warsha ya kitaalamu ambayo ilianzishwa mwaka 2008 huko mjini Soul, Korea Kusini kuhusiana na suala la 'Waislamu Waliowachache Barani Asia.' Katibu Mkuu wa OIC pia ataandaa kikao maalumu cha viongozi wa ngazi za juu wa nchi za Kiislamu katika kikao hicho cha Malaysia ili kujadili masuala mbalimbali ya pamoja ya ulimwengu wa Kiislamu.
Kikao cha 'Uchumi wa Kiislamu na Taaluma ya Kiuchumi ya Nchi za Kiislamu' kimepangwa kufanyika tarehe 28 na 29 za mwezi huu wa Aprili katika Hoteli ya Istana, sambamba na kuwadia mwaka wa 40 wa kuasisiwa Jumuiya ya Nchi za Kiislamu OIC na pia mwaka wa 25 wa kuasisiwa Chuo Kikuu cha Kiislamu cha Malaysia. 394621
captcha