Kwa mujibu wa mwandishi wa IQNA mjini Beirut, kitabu hicho kimefasiriwa kwa Kiarabu kupitia juhudi za Mwambata wa Utamaduni wa Iran nchini Lebanon.
Kitabu hicho kilichofasiriwa kwa Kirabu na Bw. Zaraqt kinatazamiwa kuanza kusambazwa katika kipindi cha siku chache zijazo.
Maudhui ya kitabu cha ‘Umahdi na Amani Kuu’ ni Imam Mahdi (as) na kina kurasa 170. Nakala ya Kifarsi ya kitabu hicho imechapishwa na Taasis ya Utafiti kuhusu Umahdi kwa ushirikiano wa Kituo cha Utafiti cha Ofisi ya Rais. 394722