IQNA

Rais Ahmadinejad, mshindi wa mkutano wa kimataifa wa Geneva

9:51 - April 27, 2009
Habari ID: 1770392
Rais Mahmoud Ahmadinejad wa Iran ndiye aliyekuwa mshindi halisi wa mkutano wa kimataifa wa kupiga vita ubaguzi huko Geneva kutokana na misimamo yake ya kishujaa, kusimama kidete na kujiami.
Hayo yamesemwa na Ayatullah Abbas Ali Sulaimani, Imam wa swala ya Ijumaa ya mji wa Zahidan nchini Iran ambaye ameongeza kuwa Rais wa Jamhuri ya Kiislamu aliwafundisha walimwengu darsa na somo la kuwatetea wananchi wanaodhulumiwa wa Palesrina na watu wanaokandamizwa kote duniani.
Amesema kuwa somo jingine lililotolewa na Rais Ahmadinejad katika kikao cha Geneva ni ushujaa ambao ni katika utamaduni wa taifa la Iran. Amesema misimamo ya kutetea haki ya Rais Ahmadinejad imezidisha uungaji mkono wa walimwengu kwa Jamhuri ya Kiislamu ya Iran. 393816

captcha