Mfuko huo umeanzishwa katika soko la hisa la Johannesburg, mji mkuu wa kibiashara wa Afrika Kusini kwa ajili ya kuhudumia jamii ya Waislamu.
Benki za Kiislamu zimewavutia watu wengi wa dini na madhehebu tofauti nchini Afrika Kusini kutokana na mfumo wa kifedha wa Kiislamu unaotumiwa katika benki hizo.
Sababu nyingi za mafanikio ya benki za Kiislamu ni uadilifu wa mfumo wa kifedha wa Kiislamu na kujiepusha kwake na riba.
Serikali na Benki Kuu ya Afrika Kusini pia zimeunga mkono mfumo wa benki ya Kiislamu nchini humo kwa kadiri kwamba Wizara ya Fedha ya nchi hiyo imeunda kamati maalumu ya kuchunguza njia za kuimarisha benki za Kiislamu. 396080