IQNA

Taasisi ya Qur'ain Thailand yatembelewa na afisa wa Iran

15:39 - April 30, 2009
Habari ID: 1771853
Mwambata wa Utamaduni wa Jamhuri ya Kiislamu ya Iran nchini Thailand, Jalal Tamleh ametembelea Kituo cha Qur'ani cha Rasul A’adham (SAW) kinachofungama na Chuo Kikuu cha Jamiatul Mustafa (SAW) al Alamiya.
Kwa mujibu wa mwandishi wa IQNA Kusini Mashariki mwa Asia, katika ziara hiyo iliyoanza kwa kisomo cha Qur'ani Tukufu, Hujjatul Islam wal Muslimin Amiri, Mwakilishi wa Chuo Kikuu cha Jamiatul Mostafa (SAW) al Alamiya nchini Thailand alimkaribisha afisa huyo wa utamaduni wa Iran katika kituo hicho. Aliwaarifisha wafanya kazi wa Kituo cha Qur'ani cha Rasul A’adham (SAW) na kubainisha kwa kifupi shughuli za taasisi hiyo.
Jalal Tamleh ameishukuru taasisi hiyo kwa harakati zake na baada ya hapo alishiriki katika uzinduzi wa kambi ya pili ya Kujifunza Qur'ani maalumu kwa vijana mabarobaro.
Amesema mafanikio yaliyopatikana katika kazi za uenezi wa dini yanatokana na msaada wa Mwenyezi Mungu SWT na baraka za Mapinduzi ya Kiislam ya Iran. Amesema mapinduzi hayo yamefanikiwa kuathiri jamii za Waislamu katika maeneo mbalimbali ya dunia chini ya muongozo wa Utawala wa Faqih.
Mwambata wa Utamaduni wa Jamhuri ya Kiislamu ya Iran nchini Thailand, Jalal Tamleh amesema ofisi yake iko tayari kushirikiana na Kituo cha Qur'ani cha Rasul A’adham (SAW) na na Chuo Kikuu cha Jamiatul Mustafa (SAW) al Alamiya.

captcha