Mkuu wa Kitengo cha Televisheni katika Shirika la Utangazaji la Jamhuri ya Kiislamu ya Iran Muhammad Hussein Sufi amemwambia mwandishi wa IQNA kuwa mbali na hayo, kumezinduliwa pia adhana zilizorekodiwa kwa umahiri na za aina yake. Amesema miaka 11 imepita bila kurekodiwa adhana mpya. Ameongeza kuwa adhana zilizorekodiwa zamani zitaendelea kutumiwa na katika siku za usoni adhana mpya zitarekodiwa kwa kuzingatia mapendekezo ya watazamaji.
396782