Duru ya tatu ya mafunzo ya urefa wa Qur'ani imepangwa kufanyika tarehe 4 Mei pambizoni mwa duru ya 11 ya mashindano ya kuhifadhi Qur'ani Tukufu ya Amir Salman bin Abdul Aziz ambayo yanasimamiwa na Wizara ya Masuala ya Kiislamu, Wakfu na Muongozo ya Saudi Arabia huko mjini Riyadh.
Kwa mujibu wa gazeti la al-Madina, mafunzo hayo yatakayowashirikisha marefa 10 wa kike na sita wa kiume yanafanyika kwa lengo la kuinua kiwango cha mashindano ya Qur'ani na kuwatayarisha marefa wa mashindano ya Qur'ani katika sehemu zote mbili za wanawake na wanaume.
Ibrahim al-Akhdhar, msimamizi wa duru hii ya mafunzo ya urefa wa Qur'ani, ameishukuru wizara iliyotajwa kwa kujihusisha na masuala ya mashindano ya Qur'ani na kuitaka iandae mashindano kama hayo katika kiwango cha kimataifa. 396853