IQNA

Mabeberu wanataka kudhibiti matukufu ya Waislamu

8:16 - May 04, 2009
Habari ID: 1773397
Mabeberu wa ulimwengu hawataki kuwapa Waislamu haki zao zitakazowafanya wastawi na kuendelea katika nyanja muhimu. Wanataka kuyadhibiti matukufu yao na kuwadhoofisha kwa kila njia.
Hayo yamesemwa na Ayatullah Taqi Mudarresi, marja' wa kidini na mwanazuoni mashuhuri wa Kiislamu huko Iraq alipokutana na kuzungumza na wanachuo wa mafunzo ya kidini, wahadhiri wa vyuo vikuu na wakuu wa makabila kutoka mikoa mbalimbali ya nchi hiyo katika mji mtakatifu wa Najaf. Amesema, mabeberu na madhalimu wa dunia katika kipindi chote cha historia wamekuwa wakitumia vibaya haja ya mwanadamu ya kuwa na mfumo wa Kisiasa na utawala bora, kwa ajili ya kuwatwisha watu mifumo isiyo ya kiuadilifu kwa lengo la kudhamini maslahi yao haramu. Amesema, mifumo fasidi na mibovu ya utawala hupelekea kubaki nyuma mataifa na kujaribu kuzuia maendeleo ya kila taifa linalojaribu kujitawala na kujitegemea. Ayatullah Mudarresi alizaliwa katika mji mtakatifu wa Karbala nchini Iraq mwaka 1945 katika familia ya maulama na watu wenye fadhila. Mwanazuoni huyo ameandika vitabu vingi ikiwemo tafsiri ya Qur'ani iitwayo Tafsiri al Hudaa yenye juzuu 18.
Kama tulivyosema mwanzoni, mwanazuoni huyo ni mmoja wa marja' taqlidi mashuhuri wa ulimwengu wa Kiislamu anayeishi katika mji mtakatifu wa Najaf nchini Iraq. 398769
captcha