IQNA

Mashindano ya Qur'ani kwa jamii za wachache nchini Saudi Arabia

8:33 - May 04, 2009
Habari ID: 1773399
Kituo cha upashaji habari za jamii za wachache wanaoishi nchini Saudi Arabia kimesema kuwa kuanzia Jumapili tarehe 3 Mei na kwa muda wa siku nne, nchi hiyo imeandaa mashindano ya Qur'ani maalumu kwa wageni wanaoishi nchini humo.
Kituo hicho kimetoa taarifa kikisisitiza kwamba mashindano hayo yataandamana na ratiba nyingine za kiutamaduni na kidini. Kwa mujibu wa gazeti la nchi hiyo la al-Ukadh, Taha Tawashi, mkuu wa kituo hicho amesema kuwa, mashindano hayo yanaendelea katika mji wa Taif chini ya anwani, 'Kigezo Chetu ni Muhmmad, Mbora wa Wanadamu.'
Amesema mpango huo utajumuisha usomaji Qur'ani, hotuba za kidini, ratiba za miongozo na malezi kwa ajili ya vijana, mashindano ya kiutamaduni na vipindi vya mafunzo kuhusu familia na jamii.
Tawashi amesema kuwa kuimarishwa kwa thamani kuu za Kiislamu na Qur'ani katika jamii pamoja na fadhila za kimaadili katika jamii ni miongoni mwa malengo muhimu ya mashindano hayo. 398733
captcha