IQNA

Kongamano la Kimataifa la Wapalestina laanza Italia

7:55 - May 04, 2009
Habari ID: 1773466
Kongamano la Saba la Kimataifa kuhusu haki ya Wapalestina kurejea katika ardhi zao zinazokaliwa kwa mabavu na Israel limeanza huko Milan Italia
Kongamano hilo ambalo linahudhuriwa na viongozi mashuhuri wa Uarabuni na Ulaya litajadili suala la ardhi za Wapalestina kukaliwa kwa mabavu na utawala haramu wa Israel. Aidha washiriki wanajadili mauaji ya umati yaliyotekelezwa na utawala dhalimu wa Israel dhidi ya watu wasio na hatia wa Ghaza hivi karibuni.
Akihutubia kongamano hilo kwa njia ya video, Waziri Mkuu wa Palestina Ismail Haniya amezitaka nchi za Ulaya kusitisha sera za kuitaja harakati ya Hamas kuwa ya kigaidi. Kongamano hilo linasadifiana na kumbukumbu ya kuikaliwa kwa mabavu Palestina tarehe 15 Mei mwaka 1948. Huo ndio uliokuwa mwanzo wa kuundwa utawala haramu wa Israel.
Siku hiyo inalaaniwa na Wapalestina kama siku ya Nakba au maafa kwani baada ya hapo Wapalestina takribani milioni moja walifukuzwa kutoka ardhi zao.
Umoja wa Mataifa unakisia kuwa Wapalestina zaidi ya milioni 4.6 wanaishi kama wakimbizi katika maeneo mbalimbali duniani. Jumuiya za Wapalestina zinasema kuwa idadi ya wakimbizi wa Kipalestina nje ya nchi ni zaidi ya milioni nane. 398326
captcha