Mkurugenzi wa Idara ya Huduma za Kibenki kwa njia ya elektorniki katika Benki ya Kiislamu ya Dubai amesema kuwa, ‘katika mpango huo, wateja wa benki wanaweza kutekeleza shughulizao za kibenki kupitia ujumbe mfupi (sms)’. Ameongeza kuwa huduma za kibenki kupitia simu ya mkononi zitawawezesha wateja kupata habari kuhusu akaunti zao kwa njia iliyo salama kabisa.
Afisa huyo wa Benki ya Kiislamu ya Dubai amesema lengo kuu la huduma hiyo mpya ni kurahisisha utekelezaji wa shughuli za kibenki.
Amesema kuwa kwa maelezo zaidi wateja wote wa Benki ya Kiislamu ya Dubai wanaweza kutembelea mtandao maaulumu wa intaneti wa benki hiyo na pia kujiandikisha ili waweze kutumia huduma hiyo mpya. Anwani ya ukurasa huo wa intaneti ni: www.alislami.ae/mobilebanking
398294