IQNA

Kupambana na ubaguzi, kigezo cha usamehevu katika Uislamu

7:56 - May 05, 2009
Habari ID: 1773987
Kuna masuala mawili muhimu ambayo yanaonekana katika vipindi tofauti vya historia ya Kiislamu. La kwanza ni kupambana na ubaguzi wa kitabaka na rangi katika jamii za Kiislamu na la pili ni uhuru wa kusema, kubainisha itikadi na haki za kiraia kwa wafuasi wa dini mbalimbali.
Hayo yamesemwa na Swaleh bin Abdul Rahman al-Haswin, mkuu anayesimamia masuala ya Haram Tukufu na Msikiti wa Mtume (saw) ulioko mjini Madina, ambaye pia ni mwandishi wa kitabu kiitwacho at-Tasamuh wal Ud'wan baina Islam wal Gharb. Amesema, inasikitisha kuwaona Wamagharibi wakiuarifisha Uislamu, ambayo ni dini ya amani na usamehevu, kuwa ni utamaduni unaotumia mabavu, ambao unawashajiisha Waislamu kutekeleza vitendo vya mabavu na ugaidi.
Katika kitabu hicho, al-Haswin amechunguza kwa kina sababu za usamehevu katika Uislamu na kusema kuwa, kimsingi zinatokana na mafundisho yake ya kidini ambapo Waislamu wanawajibishwa kuwa waadilifu na kufuatilia misimamo na mielekeo ya wastani katika jamii. Amesema kuwa maana ya usamehevu na misimamo ya wastani iliyoarifishwa na Shirika la Elimu, Sayansi na Utamaduni la Umoja wa Mataifa Unesco, inakaribia mno maana ya Uislamu ya usamehevu na udharura wa kuwepo mawasiliano kati ya wafuasi wa dini na tamaduni mbalimbali. Amesema kuwa jambo hilo liko wazi na linakubalika na wasomi na wanafikra wenye insafu wa nchi za Magharibi. 399443
captcha