IQNA

Kuvunjiwa heshima Mitume katika mchezo wa Intaneti

17:17 - May 05, 2009
Habari ID: 1774068
Msemaji wa Kituo cha Kufuatilia Masuala ya Hisia za Chuki Dhidi ya Uislamu cha Jumuiya ya Nchi za Kiislamu OIC amelezea wasiwasi wake kufuatia kusambazwa mchezo wa kompyuta unawaonyesha Mitume wa Waislamu na Wakristo wakipigana.
Katika taarifa yake, msemaji wa kituo hicho amesema kuwa mchezo huo ujulikanao kama Faith Fighter au Mpiganaji wa Kidini umesitishwa na mtandao wake kufungwa kufuatia malalamiko ya OIC.
Taarifa hiyo imesema mchezo huo unaumiza hisia za Waislamu na Wakristo na lengo lake ni kuibua chuki za kidini.
Jumuiya ya Nchi za Kiislamu yenye makao yake huko Jeddah Saudi Arabua ina nchi wanachama 57 na inawakilisha zaidi ya Waislamu bilioni moja na nusu kote duniani. 399057
captcha