IQNA

Malalamiko ya Wapalestina dhidi ya kikao kilicho dhidi ya Uislamu

9:50 - May 06, 2009
Habari ID: 1774579
Wananchi wa Palestina na baadhi ya nchi za Kiarabu wamelaani vikali uamuzi wa wabunge wenye misimamo mikali wa utawala haramu wa Israel wa kuandaa kikoa kilicho dhidi ya dini tukufu ya Kiislamu ambacho kimefanyika chini ya anwani "Chanzo cha misimamo ya kupindukia mipaka na utumiaji mabavu katika Uislamu."
Gazeti la Misri la al-Masry al-Youm limeandika kuwa wabunge hao walifanya kikao katika majengo ya bunge la utawala huo hapo siku ya Jumanne. Mzungumzaji katika kikao hicho cha uadui dhidi ya Uislamu ni Sam Solomon, Imam wa zamani wa swala ya jamaa wa msikiti wa Khartoum, mji mkuu wa Sudan ambaye aliritadi kutoka dini ya Kiislamu na kuwa Mkristo, na katika hali ya hivi sasa anahudumia maslahi ya makundi yenye misimamo mikali ya nchi za Magharibi dhidi ya Uislamu, mjini London. Wanaharakati wa Kisiasa na kiutamaduni wa Palestina wametoa taarifa wakisema kuwa Solomon hafai kuzungumzia masuala yanayohusiana na Uislamu na kwamba kuandaliwa kwa kikao hicho ni dharau ya moja kwa moja na ya wazi kwa Uislamu na Waislamu.
Wanaharakati hao wamesema kuwa lengo la kuandaliwa kikao hicho na chama cha Wazayuni wenye misimamo ya kupindukia cha Umoja wa Kitaifa ni kuchochea hisia za Waislamu.
Sam Solomon, alizaliwa katika familia ya Kiislamu nchini Sudan na kuteuliwa kuwa Imam wa msikiti mmoja mjini Khartuom kabla ya kuritadi na kuwa Mkristo anayehudumia maslahi ya maadui wa Uislamu nchini Uingereza. 400155
captcha