Kwa mujibu wa mwandishi wa IQNA Kusini Mashariki mwa Asia, Bi. Aroyo ameyasema hayo katika mkutano wake na Rais Bashar al Assad wa Syria. Amesema nchi yake inataka kujiunga na OIC kama mwanachama mtazamaji na kuongeza kuwa lengo kuu la ombi hilo ni kuunga mkono mkataba wa amani kusini mwa nchi hiyo.
Rais Aroyo ameashiria nafasi muhimu ya Syria katika eneo la Mashariki ya Kati na mikakati yake ya kusaka amani katika nchi za Kiislamu na kusema kuwa, ‘Ufilipino ina hamu ya kuimarisha ushirikiano wa kiutamaduni, kielimu na kiuchumi na Syria na itafanya kila iwezalo kufanikisha ushirikiano huo’.
Rais al Assad kwa upande wake amesema mkutano wa maafisa wa Ufilipino na Syria ni muhimu katika kuimarisha uhusiano wa pande mbili. 400772