IQNA

Umoja wa Mataifa walaani mashambulio ya utawala haramu wa Israel dhidi ya raia

11:43 - May 07, 2009
Habari ID: 1775121
Timu ya uchunguzi ya Umoja wa Mataifa imetoa taarifa ikilaani vikali mashambulio ya utawala haramu wa Israel dhidi ya vituo vya umoja huo katika Ukanda wa Gaza pamoja na kuwaua makumi ya raia waliouwa wakiwa wanatafuta hifadhi chini ya bendera ya umoja huo.
Kwa mujibu wa tovuti ya Islamonline, ripoti hiyo inakosoa na kulaani vikali mashambulio ya utawala huo katika ofisi za misaada za Umoja wa Mataifa na vilevile katika shule moja inayosimamiwa na umoja huo katika Ukanda wa Gaza, yaliyotekelezwa mwishoni mwa mwezi Disemba mwaka jana na kuendelea kwa muda wa siku 22, ambapo zaidi ya Wapalestina 40 wasio na hatia waliuawa kinyama.
Ripoti hiyo inaendelea kusema kuwa, mbali na mashambulio hayo ya kinyama kuvuruga kabisa shughuli za Umoja wa Mataifa katika Ukanda wa Gaza, pia yaliharibu na kubomoa majengo ya umoja huo na mengine ya serikali na ya mashirika yasiyo ya kiserikali, jambo ambalo lilikiuka wazi sheria za kimataifa.
Matini kamili ya ripoti hiyo, ikiwa ni siri, ilikabidhiwa kwa Baraza la Usalama la Umoja wa Mataifa hapo siku ya Jumanne. 400743
captcha