IQNA

Kikao cha 'Tafsiri katika Zama Hizi' chafanyika Saudi Arabia

11:48 - May 07, 2009
Habari ID: 1775123
Kikao cha kitaifa cha kuchunguza tafsiri mbalimbali za Qur'ani katika zama hizi kilifanyika jana Jumatano katika Chuo Kikuu cha al-Ihsan katika eneo la al-Jauf huko kaskazini mwa Saudi Arabia.
Kwa mujibu wa shirika rasmi la habari la nchi hiyo SPA, kikao hicho kimeandaliwa na Wizara ya Wakfu na Masuala ya Kiislamu kwa ushirikiano wa Kituo cha Mwongozo na Maelezo cha Jamii za Wachache nchini humo. Kimehudhuriwa na wataalamu wa masuala ya Qur'ani, wanafunzi wa Qur'ani na wawakilishi wa jamii za wachache wanaoishi nchini Saudi Arabia.
Swalih bin Nassir al-Hamoud, mmoja wa watafiti mashuhuri wa masuala ya Qur'ani wa Saudi Arabia ametoa hotuba katika kikao hicho akizungumzia umuhumu wa tafsiri katika zama hizi za teknolojia na elimu ya kisasa.
Katika kikao hicho, Abdallah bin Abdul Aziz az-Zahrani, mhadhiri wa masuala ya Qur'ani katika Chuo Kikuu cha Anas bin Malik katika eneo la al-Baha amehutubia pia kikao hicho kwa kuzungumzia wadhifa wa wafasiri wa Qur'ani.
Kiko hicho ni katika mfululizo wa shughuli za kituo kilichotajwa cha jamii za wachache nchini Saudi Arabia kwa lengo la kuwafahamisha na kuwafunza mafundisho ya kitabu kitakatifu cha Qur'ani. 400629
captcha