IQNA

‘Siku ya Uislamu’ yaainishwa Hawaii

11:09 - May 09, 2009
Habari ID: 1775712
Wajumbe katika Bunge Jimbo la Hawaii Marekani wameazimia kuahdimisha ‘Siku ya Kiislamu’ kila mwaka tarehe 24 Septemba.
Kwa mujibu wa Shirika la Habari la Time Turk la Uturuki, sheria hii imepitishwa bungeni kwa kura 22 huku kukiwa na wapizani watatu tu. Sheria hii itaanza kutekelezwa baada ya kutiwa saini na gavana wa jimbo hilo Linda Lingel.
Utangulizi wa sheria hiyo unasema hivi: ‘Dini ya Kiislamu ni dini asili na ya kihistoria. Dini hii ya Mwenyezi Mungu imejaa itikadi na maadili na hakuna yeyote anayeweza kupinga nafasi muhimu ya wafuasi wa dini hii katika kustawisha utamaduni na sanaa duniani na kwa sababu hii kuna udharura wa kutenga siku maalumu ijulikanayao kama ‘Siku ya Kiislamu’ kwa ajili ya Waisalmu wa jimbo hili’. 401556
captcha