Kwa mujibu wa Shirika Rasmi la Habari la Emarati WAM, mashindano hayo ya Quran Tukufu ambayo yanadhaminiwa Jumuiya ya Quran Tkufu ya Sharjah yatawajumuisha Mahafidh 60 wa Quran ambao ni wanachuo wa sheria, tiolojia na masomo ya Kiislamu kutoka Chuo Kikuu cha Sharjah, Chuo Kikuu cha Ajman, Chuo Kikuu cha Mafuta cha Abu Dhabi na Chuo Kikuu cha Polisi cha Dubai.
Kutakiwa na washiriki katika viwango vya kuhifadhi Quran kikamilifu, kuhifadhi juzuu 20, kuhifadhi juzuu 10, kuhifadhi juzuu tano na kuhifadhi Suratul Baqara na Suratul Ale Imran. Mashindano hayo yatamalizika tarehe 10 Mei ambapo muhadahra utatolwea na Sheikh Said Az-Ziyani mhubiri na mtaalamu wa Quran huko Emarati ambayo atazungmza kuhusu ‘Mafunzo ya Iman katika Quran’. 401530