Kwa mujibu wa ukurasa wa intaneti wa Muslim, pamoja na kuwa Wakristo wakatoliki ni asilimia tano tu ya wakaazi wa Kosovo, lakini hivi sasa wamezidisha harakati za kimishonari miongoni mwa Waislamu wa Kosovo.
Viongozi wa Kiislamu Kosovo wanasema makao ya kanisa katoloki duniani Vatican yanapanga mikakati maalumu ya kueneza Ukristo katika eneo lote la Kiislamu la Balkan kusini mwa Ulaya na Kosovo ni kati ya nchi zinazolengwa. Wanasema nchi nyinginezo zenye Waislamu wengi zilizo katika upeo wa njama za Vatican ni pamoja na Albania, Montenegro na Macedonia. Duru zinaarifu kuwa wamishonari wa Kikatoliki wanatumia vibaya na kwa maslahi yao suala la umasikini na ukosefu wa ajira miongoni mwa Waislamu. Aidha wanatumia vibaya suala ya ukosefu wa ujuzi wa mafunzo ya Kiislamu uliopo miongoni mwa wakaazi wan chi hizo za eneo la Balkan ili kueneza mafunzo batili ya Kikristo.
Amir Adami, msomi wa Albania anasema, viongozi wa kanisa Katoliki wanatumia kiasi kikubwa cha fedha ili kuwatanasarisha Waislamu.
Viongozi wa Kiislamu katika eneo la Balkan wanasema pamoja na kuwa Waislamu wa eneo hilo wanakabiliana na wamishonari lakini kuna haja kwa jumuiya na taasisi za Kiislamu duniani kuzidisha mikakati hiyo katika eneo hilo la Ulaya lenye Waislamu wengi. 400857