Mashindano ya Qur'ani kwa wanawake wa Imarati ambayo yamefanyika chini ya anwani ya Zawadi ya Hamida bint Muhammad bin Khalifa yalianza siku ya Ijumaa huko katika Kituo cha Kidini na Utamaduni cha Muhammad bin Khalid Aal Nahyan katika mji wa Abu Dhabi, ambao ni mji mkuu wa Umoja wa Falme za Kiarabu. Wanawake 57 wa Imarati waliohifadhi Qur'ani wanashiriki katika mashindano hayo.