IQNA

Kikao cha Umoja wa Kiislamu kufanyika Uturuki

12:27 - May 09, 2009
Habari ID: 1775775
Kikao cha Tatu cha Umoja wa Kiislamu ambacho kimeandaliwa na Taasisi ya Kiislamu ya Ujumbe wa Nur na kwa ushirikiano na gazeti la Asia Mpya kimeanza leo Jumamosi katika mji wa Qunia nchini Uturuki.
Kwa mujibu wa tovuti ya DunyaBulteni masuala mbalimbali yanayouhusu ulimwengu wa Kiislamu na hasa kuhusu suala la umoja wa Kiislamu katika zama hizi yatajadiliwa. Kikao hicho pia kitachunguza nafasi ya Badiu Zaman Said Nuresi, mwanazuoni na muhubiri wa Kiislamu, katika kueneza Uislamu barani Ulaya. Vikao mbalimbali vya meza duara kuhusiana na masuala ya kidini, historia ya Kiislamu na maisha ya Mtume vitaandaliwa pembeni ya kikao hicho cha siku mbili. Badiu Zaman Said Nures alizaliwa mwaka 1293 Hijiria katika kijiji cha Nures nchini Uturuki. Katika kipindi kifupi tu cha masomo yake alibobea na kupata umashuhuri mkubwa katika nyanja za hesabati, nujumu, kemia, fizikia, masuala ya ardhi, falsafa, historia na Jiografia. 401599
captcha