Ali Larijani, Spika wa Bunge la Ushauri wa Kiislamu la Iran (Bunge) ameyasema hayo Ijumaa tarehe 8 Mei alipokuwa akihutubia jopo la waandalizi wa Kongamano la Kimataifa la Kuwaunga mkono Wapalestina na kuongeza kuwa: 'Katika kadhia ya Palestina tunaona baadhi ya nchi zinachukua misimamo isiyofaa ili kuwapotosha wengine'.
Larijani amekumbusha kuwa, kuhusu kadhia ya Palestina Imam Khomeini (SA) alisema: 'Palestina ni kama ngao ya nchi zinginezo. Uwezo wao wa kujihami utabainika katika uzingatiwaji wao wa kadhia ya Palestina'.
Larijani ambaye pia ni mwenyekiti wa Kongamano la Kimataifa la Kuwanga mkono Wapalestina amesema leo katika uga wa kimataifa kunashihudiwa njama za baadhi ya nchi za kuliondoa suala la Palestina katika ramani ya masuala muhimu lakini hawajafua dafu.
Naye Katibu wa Kongamano la Kimataifa la Palestina Hujatul Islam wa Muslimin Ali Akbar Muhtashemipur amesema kongamano hilo limeweza kuakisi sauti ya Wapalestina wanaodhulumiwa hasa huko Ghaza kwa walimwengu wote. 402016