IQNA

Kuasisiwa kamati ya kutetea Quds na Islamonline

12:27 - May 11, 2009
Habari ID: 1776759
Tovuti ya Islamonline imeasisi kamati maalumu ya kutetea Quds Tukufu ili kuwadhihirishia Waislamu umuhimu wa eneo hilo takatifu. Akizungumzia suala hilo, Muhammad Zeidan, mkurugenzi wa kitengo cha lugha ya Kiingereza ya tovuti hiyo amesema kuwa kwa kubuniwa kamati iliyotajwa, tovuti hiyo ina lengo la kuwafahamisha Waislamu umuhimu, na masuala yote ya kihistoria na ya hivi sasa ya eneo hilo takatifu, ambalo linakaliwa kwa mabavu na maghasibu wa Kizayuni.
Kamati hiyo itazinduliwa rasmi wiki hii sambamba na kufanyika makumbusho ya siku ya Nakba au mkasa ambayo ni siku ya kuundwa utawala haramu wa Israel katika ardhi zilizoghusubiwa za Wapalestina mwaka 1948. Naye Kamal Badr, mhariri mkuu wa tovuti ya Islamonline amesema kuwa lengo kuu la kubuniwa kamati hiyo ni kusisitiza umuhimu wa Beitul Muqaddas na utambulisho wake wa Kiislamu. Amesema kuwa mji huo una umuhimu mkubwa kwa Wapalestina na Waislamu. Kwa msingi huo, tovuti hiyo imeanzisha ukurasa maalumu uliopewa anwani ya 'Quds, Mji wa Machungu' kwa lengo la kuonyesha historia ya mji huo na vilevile juhudi kubwa zinazofanywa na Wazayuni kwa lengo la kufuta utambulisho wa Kiarabu na Kiislamu wa mji huo na kuubadilisha na wa Kiyahudi. Zeidan amesema kuwa uzembe wa vyombo vya Kiislamu na Kiarabu katika kuzungumzia habari za Quds ni jambo ambalo limewafanya Waislamu wasijue umuhimu wa eneo hilo takatifu na hivyo kuwapelekea Wazayuni wafanye njama za kufuta utambulisho wake wa Kiislamu na Kiarabu. Utawala haramu wa Israel iliteka Quds Tukufu katika vita vya siku 6 mwaka 1967 na kulishikanisha na ardhi nyingine za Waislamu ulizokuwa umeziteka awali, kinyume kabisa na sheria za kimataifa. Tokea wakati huo hadi sasa, Israel imekuwa ikitekeleza miradi na njama nyingi za kuwafukuza Waarabu wa Palestina kutoka katika mji huo mtakatifu, kwa kubomoa nyumba na makazi yao. Wapalestina wanataraji kwamba, kupitia msaada wa Waislamu wenzao, wataweza tena kuukomboa mji huo pamoja na Msikiti wa al-Aqsa, msikiti wa tatu kwa utukufu na utakatifu katika Uislamu, na kuufanya kuwa mji mkuu wa serikali ya taifa lao huru. 402321
captcha