Ayatollah Mohammad Taqi Modaressi, mwanazuoni mwandamizi wa Kishia amesema kuheshimu haki na rai za watu katika jamii ni kati ya sifa za muhimu za jamii ya Kiislamu ambazo huipa itibari jamii inayofuata mafundisho ya Quran.
Kwa mujibu wa ukurasa wa intaneti wa almodaressi.com, Ayatollah Modaressi ameyasema hayo katika mahojiano na kanali ya televisheni ya satalaiti ya Ahlul Bayt (AS). Amesema jamii ya Qurani kamwe haiwezi kusalimu amri mbele ya madhalimu, wakandamizaji, wavamizi na wenye kiburi. Amesema jamii ya Quran itajihami mbele ya wanaouvunjia heshima Uislamu. Ameongeza kuwa iwapo jamii za Kiislamu zitazingatia mafundisho ya Kiislamu na kuifanya Quran kuwa muongozo mkuu katika harakati zote, basi jamii yenye uadilifu itaweza kubuniwa.
Ayatollah Modaressi ameashiria matatizo yaliyoko Iraq, Sudan, Lebanon, Afghanistan na Palestina na kusema: "Sisi sote kila siku tunapokea habari chungu nzima kutoka nchi hizo. Chanzo cha matatizo hayo ni kuwa Waisalmu wamejitenga na mafundisho ya Kiislamu".403516