IQNA

Kikao cha 'Hijabu, Urithi wa Mtume (saw) chafanyika

13:51 - May 12, 2009
Habari ID: 1777414
Kikao cha kitaifa cha 'Hijabu; Urithi wa Mtume (saw) kinafanyika leo Jumanne huko katika mji wa Tiaf, nchini Saudi Arabia, ambapo wanawake na wanachuo wa kike wa nchi hiyo wanashiriki.
Gazeti la nchi hiyo la Ukadh, limesema kuwa kikao hicho kinafanyika kwa ushirikiano wa Kamati ya Muamko ya Saudi Arabia. Fatima al-Jaudi, katibu wa kikao hicho amesema kuhusiana na kikao hicho kwamba, usambazwaji wa utamaduni na hijabu ya Kiislamu miongoni mwa wanawake wa Kiislamu na kuwafahamisha wanachuo wa Kiislamu hadithi za Mtume kuhusiana na umuhimu na thamani za hijabu ni miongoni mwa malengo muhimu ya kufanyika kikao hicho. Warsha ya 'Udharura na Umuhimu wa Kuvaa Hijab' imefanyika pembeni ya kikao hicho ambapo mavazi ya Kiislamu yameonyeshwa. Pia vitabu vinavyohusiana na udharura wa kulindwa heshima ya mwanamke na hijabu ya Kiislamu vimesambazwa miongoni mwa washiriki wa kikao hicho. 403274

captcha