IQNA

Uhusiano wa Uislamu na Ukristo katika karne ya 21

13:52 - May 12, 2009
Habari ID: 1777418
Kikao cha kuchunguza uhusiano wa Uislamu na Ukristo katika karne ya 21 kilifanyika siku ya Jumapili katika Kituo cha Utafiti wa Kidini cha mjini Pasadena nchini Marekani.
Kwa mujibu wa gazeti la al-Mustakbal la nchini Lebanon, katika kikao hicho, wanafikra, wataalamu na watafiti wa Kiislamu na Kikristo walichunguza kwa kina hali ya Waislamu waliowachache wanaoishi katika nchi za Kikristo na kinyume chake. Washiriki pia walichunguza na kujadili sheria za Kiislamu kuhusiana na wafuasi wa dini za wachache, sheria za kimataifa kuhusiana na haki za binadamu na hasa ya mwaka 1948 na sheria kuhusiana na jamii za wachache za mwaka 1993. Baada ya kuchunguza sheria hizo zote na kisha kuzilinganisha na za Kiislamu kuhusiana na haki za binadamu, washiriki walifikia uamuzi huu kwamba, Uislamu unaamiliana vyema zaidi na wafuasi wa dini nyinginezo za Watu wa Kitabu na hasa Wakristo na Mayahudi na kuzitambua rasmi dini mbili hizi kuwa za mbinguni. Wamesisitiza juu ya kulidwa haki za Waislamu waliowachache katika nchi za Kikristo na kinyume chake na kuongeza kwamba mbali na itikadi za kidini za mwanadamu, mwanadamu huyo anapasa kuheshimiwa kama mtu aliyerithishwa masuala mengi humu duniani na Mwenyezi Mungu. Wameashiria kwamba suala la kuheshimiwa haki za binadamu, utukufu na nafasi yao muhimu katika jamii limesisitizwa mno katika matini za Kiislamu. Takriban thuluthi moja ya Waislamu wanaishi kama jamii za wachache katika nchi zisizo za Kiislamu kama vile India, Russia, Uchina na nchi ngingine za Ulaya na Latin Amerika. Nao Wakristo ambao hadi karne ya 19 walikuwa wakiishi kwa wingi katika nchi za Ulaya na Amerika Kaskazini, hivi sasa wanaunda thuluthi moja katika mabara ya Asia, Afrika na Latin Amerika, jambo ambalo limewapelekea kuishi pamoja kwa amani na ushirikiano na Waislamu. 403366
captcha