IQNA

Mawahabbi wanajidhuru kwa tuhuma zao dhidi ya Ushia

11:18 - May 13, 2009
Habari ID: 1777625
Mkuu wa Masuala ya Kimataifa katika Chuo Kikuu cha Jamitul Mostafa (SAW) al Alamiya ameashiria matamshi ya kuwakufurisha Mashia ya Imam wa Jamaa wa Msikiti Mtukufu wa Makka na kusema: “Tuhuma za Mawahabbi dhidi ya Madhehebu ya Kishia hazina natija nyingine isipokuwa kuharibu sura ya Mawahabbi wenyewe katika uga wa kimataifa”.
Kwa mujibu wa mwandishi wa IQNA, Hujjatul Islam wa Muslimin Hakimilahi Mkuu wa Masuala ya Kimataifa katika Chuo Kikuu cha Jamitul Mostafa (SAW) al Alamiya Jumatatu Mei 12 ameongeza kuwa kwa matamshi yake hayo, Imam wa Jamaa wa Msikiti Mtukufu wa Makka ameuthibitisiha ulimwengu uliostawi kielimu kuwa yeye ni mtu aliye nyuma sana katika zama hizi za teknilojia mpya ya mawasiliano na kwamba ameghafilika kunufaika na fikr za wanaadamu. Amesema zama za kutoa tuhuma za uongo ili kuwaondoa washindani katika medani ni mbinu ya kale isiyotumika tena.
Mkuu huyo wa Chuo cha Kiislamu cha London ameashiria utajiri katika Utamaduni wa Watu wa Nyumba ya Mtume (SAW) - Ahul Bayt (AS) -na kusema, hivi sasa kuna wimbi kubwa la Waislamu wa madhehebu yote na hata wasio kuwa Waislamu kuvutiwa kwa kiasi kikubwa na Mafunzo ya Ahul Bayt (AS).
Mwanazuoni huyo ametoa wito kwa Mashia wote wafuasi wa Ahlul Bayt (AS) kunyoosha mkono wa umoja kwa Waisalmu wote. Hujjatul Islam wa Muslimin Hakimilahi amesema Maulamaa na wanafikra wa Kiislamu wana jukumu la kukabiliana na Mawahabbi ambao wanayavunjia heshima matukufu ya Waislamu wengine.
Kwingineko, Sheikh Abbas Ka'abi Mjumbe wa Baraza la Wanazuoni linalomchagua Kiongozi Muadhamu katika Jamhuri ya Kiislamu ya Iran amesema kuwa, serikali ya Saudi Arabia inapaswa kumfuta kazi Imam wa Jamaa wa Msikiti Mtukufu wa Makka aliyewavunjia heshima Waislamu wa Madhehebu ya Shia, na kupaza sauti ya kishetani kwenye ardhi ya wahyi. Sheikh Abbas Ka'abi amelaani kitendo hicho cha Sheikh Adel Kalbani na kuongeza kuwa, ilitegemewa kusikika katika minbar za ardhi za wahyi na ndani ya al Kaaba sauti ya umoja na mshikamano wa umma wa Kiislamu katika kukabiliana na maadui wa Kiislamu, Wazayuni wa kimataifa na viongozi wa Marekani; amma inasikitisha kuona kwamba hivi sasa inasikika sauti ya kishetani na yenye kuleta fitna na mifarakano kati ya Waislamu. Akizungumzia vitendo vya udhalilishaji vinavyofanywa na askari wa Saudi Arabia dhidi ya waumini wa Kiirani na hasa wanawake wanaokwenda kufanya ibada ya U'mra, Sheikh Ka'abi ameongeza kuwa, viongozi wa serikali ya Iran wanapaswa kuchukua hatua madhubuti katika kukabiliana na vitendo hivyo, kinyume cha hivyo zitachukuliwa hatua za kususia U'mra kama walivyopendekeza Maraji'i wa kidini nchini Iran. 403778
captcha