IQNA

Kikao cha 7 cha Baraza la Kiislamu cha Eurasia chaanza Istanbul

11:19 - May 13, 2009
Habari ID: 1777638
Mkutano wa saba wa Baraza la Kiislamu la Eurasia kimeanza Jumanne mjini Istanbul kwa himaya ya Wizara ya Masuala ya Kidini ya Uturuki.
Kwa mujibu wa gazeti la Yeni Safak, Ali Barakoghlu Waziri wa Masuala ya Dini wa Uturuki amesema zaidi ya maulamaa 80 , wasomi na wanafikra wa kidini kutoka nchi 42 wanashriki katika kikao hicho.
Ameongeza kuwa, dini haipaswi kuwa kutumiwa kuibua unafiki na mifarakano kwani asili ya dini ni kuleta umoja baina ya wanaadamu na kuwakurubisha wanaadamu kwa Mwenyezi Mungu. Kwa hivyo lengo la mkutano huo ni mazingmzo kwa lengo la kuleta ukuruba kwa msingi wa nukta za pamoja.
Barakoghlu amesema mkutano huo utaendelea kwa muda wa siku tatu na kwamba washiriki hawatakuwa na lengo ila kuleta umoja miongoni mwa Waislamu wa eneo la Asia na Ulaya. Ameongeza kuwa ili kufikilea lengo tukufu la umoja, hakuna Muislamu anayeppaswa kujiona kuwa bora zaidi ya wengine kwani moja ya hatua za awali za ukuraba katika uhusiano ni kufahamiana na kuheshimu itikadi za kila moja. 403847
captcha