Masomo hayo yanatazamiwa kuanza tokea tarehe 24 Mei huko mjini Jeddah. Kwa mujibu wa gazeti la Saudi Gazzette, masomo hayo yameandaliwa kwa ajili ya kuwafunza masomo maalumu wakuu wa benki za Kiislamu na pia kuwawezesha wakuu hao kutathmini hatari, rekodi na kuchukua uamuzi unaofaa katika nyanja za huduma za fedha za Kiislamu. Wanachuo wa vyuo vikuu pia watafahamishwa mbinu mbalibali za sekta ya fedha ya Kiislamu kwa ajili ya kuboresha huduma za kifedha kwa wateja. Haifa Jamal Alyal, Mkuu wa Chuo Kikuu cha Iffat amesema kuhusiana na suala hilo kwamba, kuandaliwa kwa duru hiyo ya masomo ni fursa ya dhahabu kwa ajili ya kuungwa mkono na kuimarishwa taasisi za kifedha za Kiislamu na kuondoa pengo lililopo kati ya vyuo vikuu na mahitaji ya jamii. 404605