Kwa mujibu wa shirika rasmi la habari la Bahrain GNA, kikao hicho kimeandaliwa na Benki ya Ustawi ya Kiislamu ambapo wawakilishi na wanauchumi pamoja na wataalamu wa masuala ya kifedha ya Kiislamu kutoka nchi mbalimbali za dunia zikiwemo za Russia, Ulaya, Mashariki ya Kati na za kusini mashariki mwa Asia wanatazamiwa kushiriki. Kuchunguzwa suhula, matarajio na shughuli za benki za Kiislamu huko Russia, njia za kuimarisha ushirikiano wa kiuchumi wa Russia na ulimwengu wa Kiislamu na mabadilishano ya biashara kati ya taasisi za kifedha na benki za Kiislamu na benki za Ruusia ni baadhi ya mambo yaliyopangwa kujadiliwa katika kikao hicho. 404511