IQNA

Kikao cha masuala ya uchumi cha OIC mjini Ezmir

14:12 - May 14, 2009
Habari ID: 1778289
Kikao cha 25 cha kimataifa cha masuala ya kiuchumi kilichaondaliwa na Kamati ya Kudumu ya Ushirikiano wa Kiuchumi na Kibiashara ya Umoja wa Nchi za Kiislamu OIC kilianza siku ya Jumanne mjini Ezmir Uturuki.
Kikao hicho kimefunguliwa kwa hotuba za mkuu wa kamati hiyo, rais wa Uturuki pamoja na katibu mkuu wa umoja huo wa OIC. Rais Abdallah Gul amesisitiza katika ujumbe wake kwa kikao hicho, juu ya ulazima wa kuimarishwa ushirikiano kati ya nchi za Kiislamu. Amesema kuwa nchi wanachama wa OIC zinapasa kunyanyua kiwango chao cha ushirikiano wa kibiashara na kiuchumi katika ngazi za kimataifa na kutafuta uwekezaji mpya kutoka pembe mbalimbali za dunia. Kwa upande wake, Ikmal Deen Ihsanoghlou, Katibu Mkuu wa Umoja wa Nchi za Kiislamu OIC ameashiria katika ujumbe wake mgogoro wa kiuchumi unaoendelea katika pembe mbalimbali za dunia, kuongezeka kwa bei ya mahitaji muhimu na athari za kupungua bei ya mafuta kwa nchi za Kiislamu wanachama wa OIC na kusisitiza kuwa, nchi hizo zinapasa kushirikiana zaidi ili kuboresha hali yao ya uchumi. Kikao hicho kinatazamiwa kumalizika leo Alkhamisi. Kamati ya Kudumu ya Ushirikiano wa Kiuchumi na Kibiashara ya OIC iliasisiwa mwaka 1981 katika duru ya tatu ya kikao cha viongozi wa umoja huo mjini Makka. Lengo lake kuu ni kuimarisha ushirikiano wa kiuchumi kati ya nchi za Kiislamu. 404494
captcha