Muhammad ad-Dureini, mkuu wa taasisi hiyo mjini Cairo Misri na Wa'd al-Husseini, mar'ja' wa Kishia ambaye pia ni mkuu wa taasisi ya al-Beit (as) mjini Baghdad wametoa taarifa ya pamoja wakisisitiza kwamba watawashtaki mamufti hao wa Saudia katika mahakama liliyotajwa kwa kosa la kutoa fatuwa ya jinai dhidi ya binadamu na kukufurisha Mashia. Amesema tayari mashtaka yameshatayarishwa na kwamba yatawasilishwa hivi karibuni kwa mahakama iliyotajwa. Wa'd al-Husseini amesisitiza kuwa kukufurishwa mashia na kushajiishwa makundi ya kisalafi na Kiwahabi kumwaga damu ya Mashia ni jambo linalokwenda kinyume kabisa na maazimio pamoja na sheria za kimataifa na kuhesabiwa kuwa jinai dhidi ya binadamu, na kwamba mamufti waliotoa fatuwa hiyo wanapaswa kushughulikiwa kisheria na kufikishwa mbele ya mahakama. Amesema fatuwa kama hizo zilizotolewa huko nyuma na mamufti hao wa kisalafi na Kiwahabi zimepelekea kuuawa na kumwagwa damu ya maelfu ya Wairaki wasio na hatia na vilevile kuzidisha ghasia na machafuko nchini humo, na kwamba taasisi ya Aali Beit itatumia jambo hilo kama dalili muhimu ya kuhukumiwa mamufti hao wa Saudia katika mahakama ya kimataifa. Katika mahojiano na televisheni ya BBC wiki iliyopita, Adil al-Kalbani, Imam wa Msikiti Mtukufu wa Makka, alitoa matamshi ya kipumbavu na chuki dhidi ya Mashia kwa kuwakufurisha na kuhalalisha umwagaji wa damu yao. 404479