Katika mkutano wake na Waziri wa Mambo ya Nje wa Oman Yusuf Bin Alawi, Spika wa Bunge la Iran Ali Larijani amesema kuna udharura wa uhusiano wa nchi za Kiislamu katika kutatua migiroro ya kieneo na kuongeza kuwa, 'uhusiano wa Tehran na Muscat haupaswi kubakia katika kiwango cha sasa bali unapaswa kupanuliwa zaidi'.
Larijani ameendelea kusema kuwa kuna haja ya kuimarishwa uhusiano baina ya nchi za Kiislamu katika kutatua migogoro ya kieneo. Larijani pia amekutana na kufanya mazungmzo na Mfalme wa Oman Sultan Qaboos. 403888