Katika kipindi cha miaka mine iliyopita, duru kama hizo za masomo ya Qur'ani zimekuwa zikiendeshwa na walimu wenye uzoefu mkubwa katika usomaji wa Qur'ani ambao wanasimamiwa na Hujjatul Islam wal Muslimeen Dhakir Hussein Irfani, ambaye amehitimu masomo yake katika Kituo cha Kimataifa cha Mustafa (saw) mjini Qum. Kwa mujibu wa ripoti hiyo, hivi sasa pia mwanafunzi mwingine wa kike aliyehitimu masomo yake katika Chuo Kikuu cha az-Zahra cha mjini Qum nchini Iran, kila siku hutoa mafundisho ya Qur'ani kwa wanafunzi wa kike na kiume katika eneo hilo la Gilgit. 405494