Kama zilivyokuwa duru nyingine za maonyesho ya vitabu ya mjini Tehran, duru hii ya 22 ya maonyesho hayo ya vitabu pia imeshuhudia vitabu mbalimbali vipya vinavyozungumzia Qur'ani na masuala mengine mengi ya Kiislamu.
Vitabu hivo vinaonekana kwa wingi katika vibanda vya vitabu vya nchi za India, Lebanon na Misri. Shirika muhimu zaidi la vitabu la India ambalo limewasilisha vitabu vyake katika duru hii ya maonyesho ni shirika la Orient ambalo linaonyesha vitabu mbalimbali vya masuala ya kielimu, kisheria, kiutamaduni na Kiislamu. Kuhusiana na sekta ya vitabu vya Kiislamu, kitabu ambacho kinavutia macho zaidi katika kibanda hicho ni kile cha Encyclopedia of Islamic Economy. Kitabu hicho kinahusiana na masuala mbalimbali ya kiuchumi na kifedha, biashara na maana ya uchumi wa Kiislamu, ushirika na umiliki na mifumo ya benki za Kiislamu. Kitabu kingine muhimu kinachoonekana katika kibanda hicho ni kile cha Famili Law in Islam kinachohusiana na familia katika Uislamu ambacho kimeandikwa na Arif Ali Khan. Kitabu hicho kinabainisha kwa kina sheria za Kiislamu kuhusiana na masuala ya kijamii, kifamilia na kimaadili, haki za wazazi, watoto, majirani na za mume na mke katika ndoa.404828