Kikao hicho kimeandaliwa na Shirika la Elimu, Sayansi na Utamaduni la Umoja wa Mataifa Unesco kwa ushirikiano wa Wizara ya Utamaduni ya Senegal, kwa shabaha ya kuandaa mazingira ya kuishi pamoja kwa amani wafuasi wa dini tofauti. Viongozi wa dini mbalimbali wanatazamiwa kushiriki katika kikao hicho. Kitawajumuisha viongozi na wawakilishi kutoka nchi za Banin, Ivory Coast, Gambia, Guinea Bissau, Ghana, Mali, Nigeria, Senegal na Cape Verde. Viongozi na washiriki wa kikao hicho cha Dakar wanatazamiwa kujadili nukta za udhaifu na vikwazo vinavyozuia kufanyika mazungumzo kati ya dini mbalimbali na hasa kati ya Uislamu na Ukristo pamoja na kutafuta njia za kuimarisha uhusiano wa wafuasi wa dini mbili hizi muhimu za mbinguni. 405381