IQNA

Baraza la Maulama wa Bahrain lalaani kukufurishwa Mashia

12:58 - May 17, 2009
Habari ID: 1779313
Baraza la Wazauoni wa Bahrain limetoa taarifa likilaani vikali hatua ya baadhi ya mamufti wenye misimamo ya kupindukia mipaka wa Kihabui wa nchini Sauadi Arabia ya kuwakufurisha wanazuoni wa Kishia na kutoa wito wa kuuawa wafuasi wa madhehebu hii muhimu ya Kiislamu, na kusema kuwa fatuwa zinazotolewa na mamufti hao ni katika kudhamini malengo ya maadui wa Uislamu.
Taarifa hiyo imesema kuwa matamshi na fatuwa hiyo iliyotolewa na baadhi ya mamufti wa kiwahabi wa Saudia akiwemo Adil Alkalbani, Imamu wa Msikiti takatifu wa Makka ni mitazamo ya kundi la wachache ambayo haitakuwa na athari yoyote katika kuvuruga juhudi kubwa ambazo hadi sasa zimefanyika kwa lengo la kuleta umoja na mshikamano miongoni mwa Waislamu wote. Taarifa hiyo imeendelea kusema kuwa katika hali ya hivi sasa, ulimwengu wa Kiislamu unakabiliwa na changamoto nyingi za kiutamaduni, kifikra, kijamii, kimaadili, kiuchumi na kisiasa na kwamba ni umoja tu ndio utakaowawezesha Waislamu kukabiliana na changamoto hizo. Baraza hilo la wanazuoni limelaani vikali matamshi na fatuwa zisizo za kimantiki zinazotolewa na mamufti wa kiwahabi wa Saudia na kusisitiza kuwa fatuwa hizo za kitaasubi hazihudumii maslahi ya umma wa Kiislamu na kwamba zinachochea tu mifarakano na fitna za kimadhehebu miongoni mwa Waislamu kwa maslahi ya maadui wa Kiislamu. Baraza hilo limewataka Waialamu wote kusimama kidete dhidi ya maadui wa Kiislamu wanaoimarisha ubeberu na njama dhidi ya nchi za Kiislamu, na wakati huohuo kushikamana kwa madhumuni ya kukabiliana na njama za utawala haramu wa Israel katika kitovu cha ulimwengu wa Kiislamu. 405750
captcha