IQNA

Kuchomwa moto Qur'ani katika kampeni za uchaguzi nchini Norway

14:10 - May 18, 2009
Habari ID: 1779721
Chama cha Taifa cha Norway ambacho ni moja ya vyama vyenye misimamo ya kupindukia mipaka nchini humo kina nia ya kuchomo moto, hadharani na mbele ya vyombo vya habari, Qur'ani Tukufu katika moja ya mikusanyiko yake ya kampeni za uchaguzi wa kuwania viti vya Bunge la Ulaya.
Chama hicho bila ya kuwa na haya wala woga kimetangaza kwamba kitatekeleza kitendo hicho cha chuki dhidi ya Uislamu ili kuwavutia wapiga kura wanaopinga dini hii tukufu nchini humo, na kwamba imekwishatiliana saini mkataba wa kuonyesha moja kwa moja picha na shughuli za uchomaji moto huo wa Qur'ani na shirika moja la televisheni ya satalaiti la nchi hiyo. Lakini katika kutoa radiamali yake kuhusiana na kitendo hicho, cha dharau dhidi ya Qur'ani na matukufu ya kidini, Abdul Sami' an-Nasri, Mkuu wa Kitengo cha Uhubiri cha Umoja wa Jumuiya za Kiislamu barani Ulaya amesema kuwa, kwa bahati mbaya kitendo hicho cha chuki cha chama kilichotajwa cha Norway kinaungwa mkono kikamilifu na Rond Giskes, Waziri wa Utamaduni wa nchi hiyo. Amesema, hali hii inatokana na ukweli kwamba waziri huyo ametoa krone milioni kumi za Norway kwa Televisheni ya Uhuru ili kutangaza kwa uhuru kamili shughuli za vyama vya upinzani vya nchi hiyo. Amesema Waziri huyo amechukua hatua hiyo kwa kisingizio cha kuunga mkono uhuru wa kusema na kwamba hiyo ni njia moja ya kulalamikia kuongezeka kwa kasi idadi ya Waslamu barani Ulaya. Katika upande wa pili, Abid Rajaa, mwanachama wa chama cha Liberal cha Norway amesema kuwa kutolewa kibali cha kuchomwa moto Qur'ani hadharani tena mbele ya vyombo vya habari ni jambo linalokiuka wazi katiba ya nchi hiyo na kusisitiza kwamba jambo hilo bila shaka litazidisha chuki kati ya jamii mbalimbali za nchi hiyo. Uchaguzi wa Bunge la Ulaya umepangwa kufanyika tarehe 4 hadi 7 za mwezi Juni ujao katika nchi 27 wanachama wa Umoja wa Ulaya. 406267
captcha