IQNA

Kikao cha 'Quds Yalia, Palestina Yapambana' chafanyika nchini Uturuki

14:06 - May 18, 2009
Habari ID: 1779722
Kikao cha 'Quds Yalia, Palestina Yapambana', ambacho kimeandaliwa na Jumuiya ya Kuunga Mkono Palestina kilifanyika siku ya Jumamosi huko katika mji wa Adana nchini Uturuki kusini mwa Uturuki.
Akizungumza katika kikao hicho, Abdul Rahman DailiPak mwandishi magazeti wa Uturuki amesema kuwa si Waislamu ndio watakaoikomboa Palaestina na Msikiti wa al-Aqsa bali ni msikiti huo ndio utakawabainishia Waislamu njia ya kuwakwamua na kuwakomboa kutoka kwenye dhulma. Amesisitiza kwamba Mwenyezi Mungu atawaadhibu vikali madhalimu kupitia mtihani huo mkubwa. Amesema, ni Waislamu ndio wanauhitajia Msikiti wa al-Aqsa na kwamba iwapo Mwenyezi Mungu ataona maslahi, atatuma askari Wake wasioonekana ili kuwasaidia Wapalestina madhulumu dhidi ya madhalimu wa Kizayuni. Amesema, katika hali hiyo, Waislamu watapewa mtahani mkubwa wa kusimama kidete mbele ya hujuma ya madhalimu na hivyo kuthibitisha kwamba hawasalimu amri mbele ya ukoloni na ubeberu. Katika sehemu nyingine ya hotuba yake kwenye kikao hicho, DailiPak amesisitiza kwamba juhudi za kukomboa msikiti wa al-Aqsa ni jukumu la kila mtu mwenye fikra huru na ya kupigania haki na kuongeza kwamba, suala la kuwasidia Wapalestina waondokane na udhia pamoja na mateso ya maghasibu wa Kizayuni ni jukumu la wapigania uhuru wote ulimwenguni. 406290
captcha