Lego la kiko hicho limetajwa kuwa ni kuarifishwa mchango wa Imam Ali na Ahlul Beit (as) kwa ujumla katika kuhuisha na kueneza Uislamu duniani. Kuchunguzwa maisha ya Imam Ali (as) na fikra pamoja na mitazamo yake kuhusiana na jinsi ya kumfahamu Mwenyezi Mungu ni baadhi ya mambo yatakayochuguzwa katika kikao hicho. Huku akiashiria umuhimu wa kuchunguzwa maisha ya Mtukufu Imam Ali na Uhlul Beit (as) kwa ujumla, Wali Guler, mmoja wa waandaaji wa kikao hicho amesema kuwa maisha ya Imam Ali (as) pamoja na ya Watu wote wa Nyumba ya Mtume Muhammad (as) ni jambo ambalo limekuwa likifuatiliwa kwa karibu na Waislamu katika kipindi chote cha maisha ya watukufu hao. Amesema jambo hilo linatokana na ukweli kwamba baada ya Mtume Muhammad (saw), Imam Ali (as) ndiye mtu aliyetoa mchango mkubwa zaid katika kueneza Uislamu duniani. Amesema maisha ya Imam Ali (as) na jinsi alivyoamiliana na maadui wa Uislamu ni jambo ambalo daima limekuwa likizingatiwa na Waislamu na wasio Waislamu na kwamba Waislamu wote bila ya kujali Ushia na Usuni wao wana jukumu la kutwalii na kuchukua maisha yake kuwa mfano bora wa kuigwa. 406328