IQNA

Wakristo wa Iraq walaani kukufurishwa Mashia

14:11 - May 18, 2009
Habari ID: 1779728
Wakristo wa Iraq wametoa taarifa wakilaani vikali hatua iliyochukuliwa na idadi kadhaa ya mamufti wa Saudi Arabia ya kukufurisha wanazuoni wa Kishia pamoja na kuhalalisha umwagwaji damu ya wafuasi wa madhehebu ya Shia.
Wakristo hao walikusanyika siku ya Jumamosi katika mitaa ya mji wa Babel na kukemea vikali maneno ya kipumbavu ya Adil al-Kalbani Imam wa Msikiti Mtukufu wa Makka dhidi ya wanazuoni wa Kishia. Akizungumza kuhusiana na suala hilo, Sami Wakil, Askofu wa Kanisa la Mtakatifu Maryam (sa) la mjini Babel amesema kwamba, uchochezi wa al-Kalbani unatekelezwa katika fremu ya njama za maadui za kudumisha ghasia na machafuko nchini Iraq na hivyo kuleta mgawanyiko kati ya makundi mablimbali ya nchi hiyo. Amesema kuwa matamshi ya kitaasubi ya Imam huyo bila shaka yatazusha hitilafu na kuvuruga kabisa umoja wa ulimwengu wa Kiarabu. Askofu Wakil amekemea vikali matamshi hayo ya al-Kalbani na kusisitiza kuwa, Wakristo wa Iraq daima wamekuwa wakiheshimu wafuasi wa makundi mbalimbali ya kidini na kimadhehebu nchini humo, yakiwemo ya Mashia na Masuni. Idadi kadhaa ya manazuoni wa kisalafi na kiwahabi wa Saudi Arabia hivi aribuni walitoa fatuwa ya kichochezi na kitaasubi wakiwakufurisha maulamaa wa Kishia na kuhalalisha umwagwaji wa damu ya wafuasi wa Ushia. 406356
captcha