IQNA

Mufti wa Tunisia akabidhiwa vitabu vya Imam Khomeini (SA)

13:52 - May 20, 2009
Habari ID: 1780674
Mwambata wa Utamaduni wa Jamhuri ya Kiislamu ya Iran amemkabidhi Mufti wa Tunisia Sheikh Uthman Batih vitabu vya Fiqhi vya Imam Khomeini (AS).
Kwa mujibu wa mwandishi wa IQNA vitabu hivyo vimetunukiwa kwa munasaba wa mwaka wa 20 wa kuaga dunia Mwanzilishi wa Jamhuri ya Kiislamu ya Iran. Lengo limetajwa kuwa ni kuarifisha fikra na mitazamo ya Imam Khomeini (SA) kwa Mufti wa Tunisia.
Kati ya kazi nyingine zilizofanya na Idara ya Mwambata wa Utamaduni wa Jamhuri ya Kiislamu ya Iran huko Tunisia ni pamoja na kusambaza CD ya Wasia wa Imam Khomeini (SA) kwa lugha ya Kifaransa katika balozi zote za kigeni mjini Tunis pamoja na vituo mbali mbali vya utamaduni nchini humo.
Aidha idara hiyo imechapisha upya kitabu kuhusu Maisha ya Imam Khomeini (SA) kilichoandikwa na Ghulamali Rajadi kwa lugha ya Kiarabu. 407862
captcha